Msanii wa nyimbo za injili nchini Kenya, Ringtone Apoko, amezua mapya baada ya kujigamba na kusema kwamba ndiye msanii tajiri zaidi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akizungumza na Mpasho Rigntone alidai kwamba kitu ambacho staa wa Bongo Diamond Platnumz amemshinda nacho ni kuwa na wafuasi wengi mitandaoni na uchawi.

“Kitu pekee ambacho Diamond ananishinda ni wafuasi na uchawi tu. Linapokuja suala la pesa na maisha makubwa mimi niko mbele yake sana. Mwambie anifanyie uchunguzi. Pesa ya Kenya ina nguvu kuliko fedha ya Tanzania,” Ringtone Alizungumza.

Huku akizungumzia siasa alisema kuwa;

“Nina marafiki zaidi ya 20 ambao ni wanasiasa lakini nina ushawishi zaidi kuliko wao. Nilidhani kwa kujiunga na siasa unakuwa na ushawishi zaidi lakini sivyo.

Eric Omondi ana nguvu zaidi kwa sababu ana sauti kubwa zaidi, Sauti Sol nawapenda pia lakini nachukia jinsi wanavyopenda wanawake wanaochumbia. Lakini ushawishi walio nao ni mkubwa sana ikilinganishwa na kama wangekuwa kwenye siasa.”